Jumanne, 3 Novemba 2015

Watanzania wengi kwa ujumla wao wanashangilia na kushabikia wito wa kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa 25/10/2015 bila hata kuwa na uhakika wa kile kinachowafanya waandamane, wanaamini tu kila kinachosemwa na UKAWA hata kama kimefinywangwa tu.
Kwa kuwa suala ni kuamini tu, basi waamini tu na ule upande wa pili.
WAMEBANIKWA KWA AJILI YA HASARA YA BAADAYE.

MAZINGIRA HAYA SI SALAMA KWETU

Unapoingia barabarani kuandamana kupinga unachopinga, Viongozi Wakuu wa Chama si sehemu ya Waandamaji. Hawa huandaa na kuhamasisha maandamano kwa nguvu kubwa ya kupinga MAZUIO yote ya Serikali na kutengeneza MGOGORO kati ya Waandamanaji na vyombo vya DOLA ya kufurumishana na kulipuliwa mabomu. Viongozi wanakuwa wametangulia kwenye viwanja vya mikutano na hotuba zao MIKOBANI kusubiri kupokea na kuhutubia WAANDAMAJI tu. Mazingira haya ni kutolewa KAFARA na Wanasiasa kwa maslahi binafsi ya WANASIASA. JITENGE NA MATAMKO YA USHIKINIZI YA WANASIASA, si salama.