Jumanne, 3 Novemba 2015

Watanzania wengi kwa ujumla wao wanashangilia na kushabikia wito wa kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa 25/10/2015 bila hata kuwa na uhakika wa kile kinachowafanya waandamane, wanaamini tu kila kinachosemwa na UKAWA hata kama kimefinywangwa tu.
Kwa kuwa suala ni kuamini tu, basi waamini tu na ule upande wa pili.
WAMEBANIKWA KWA AJILI YA HASARA YA BAADAYE.

MAZINGIRA HAYA SI SALAMA KWETU

Unapoingia barabarani kuandamana kupinga unachopinga, Viongozi Wakuu wa Chama si sehemu ya Waandamaji. Hawa huandaa na kuhamasisha maandamano kwa nguvu kubwa ya kupinga MAZUIO yote ya Serikali na kutengeneza MGOGORO kati ya Waandamanaji na vyombo vya DOLA ya kufurumishana na kulipuliwa mabomu. Viongozi wanakuwa wametangulia kwenye viwanja vya mikutano na hotuba zao MIKOBANI kusubiri kupokea na kuhutubia WAANDAMAJI tu. Mazingira haya ni kutolewa KAFARA na Wanasiasa kwa maslahi binafsi ya WANASIASA. JITENGE NA MATAMKO YA USHIKINIZI YA WANASIASA, si salama.

Jumamosi, 24 Oktoba 2015

NI KWA NINI MBOWE HATAKI KUFUATA KANUNI ZA UCHAGUZI?

Kwa wafuasi wa CHADEMA/UKAWA, kwa Watanzania wote kwa ujumla na kwa Wadau wote wa uchaguzi NI KWA NINI M/Kiti wa CHADEMA MH. Freemam Mbowe kwa nguvu zote na muda wote AMESISITIZA kutokuwa na IMANI na sheria na kanuni zinazotawala mchakato mzima wa uchaguzi?
-Kuna majibu mengi hadi yale ya kijinga lakini kubwa ni lile la HOFU YA KUSHINDWA URAIS Mgombea wake na CHADEMA kusambaratika kutokana na mabadiliko aliyoingiza ndani ya CHADEMA.
Wananchi puuzeni "KULINDA KURA", pigeni kura, ondokeni kwa amani na pokeni matokeo kwa amani.

Alhamisi, 8 Oktoba 2015

NO ROOM FOR FICTIOUS DRAMA!

In my innermost sense of understanding, I hate all fictious and Utopian POLITICAL platform DIALOGUES.

Jumanne, 6 Oktoba 2015

UCHAGUZI NI MCHAKATO WA UPINZANI

Watanzania waelewe wazi kuwa uchaguzi ni mchakato wa ushindani kupitia KAMPENI na mwisho upigaji KURA. Hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kuwa ni lazima ataibuka MSHINDI. Kuwaaminisha wafuasi na mashabiki kuwa ushindi ni lazima, ni kutengeneza mazingira ya kutokuwa na IMANI kwa vyombo vya USIMAMIZI wa Uchaguzi. HAPA ni vema kuheshimu hatua zote za uchaguzi.